Loading...

Rais Magufuli Amfukuza Kazi Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi na kumfukuza kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Faisal Issa kutokana na utovu mkubwa wa nidhamu aliouonesha katika kikao cha kamati ya ulinzi kilichofanyika tarehe 15 Januari, 2016 Mjini Mwanza.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya yaliyotokea katika kikao cha kamati ya ulinzi cha Mkoa, kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
15 Januari, 2016



Source: GPL
Rais Magufuli Amfukuza Kazi Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza. Rais Magufuli Amfukuza Kazi Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza. Reviewed by Zero Degree on 1/16/2016 10:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.