Loading...

CCM kujaza nafasi za waliotimkia Ukawa


Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa wagombea watakaoziba nafasi za uenyekiti katika mikoa ya Arusha, Shinyanga na Singida, waliohama chama chicho na kujiunga na Ukawa.

Wenyeviti hao ni Khamis Mgeja (Shinyanga), Onesmo Ole Nangole (Arusha) na Mgana Msindai (Singida) waliohamia Chadema kwa nyakati tofauti, wakati wa mchakamchaka wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ulipokuwa umepamba  moto nchini.

Mbali na hao nafasi nyingine ambazo zitazibwa baada ya kuachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya viongozi kuihama CCM na vifo ni zile za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na uenyekiti wa CCM wilaya.

Pia, nafasi ya katibu wa uchumi na fedha Mkoa wa Kilimanjaro, katibu wa siasa na uenezi wa Mkoa wa Arusha na uenyekiti wa umoja wa vijana CCM mkoa nazo zitazibwa.

Akizungumzia kuhusu uteuzi huo jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa, ilikuwa na kikao maalumu cha siku moja juzi na kufanya kazi hiyo.

Alisema katika kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete waliteua wagombea wa nafasi mbalimbali zilizo wazi za uongozi ndani ya chama, mikoani na wilayani. Ratiba ya uchaguzi huo itatolewa mwishoni mwa wiki hii.

Aliwataja wagombea uenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha kuwa ni Michael Lekule, Emanuel Lusenga na John Pallangyo.

Wagombea wa nafasi hiyo mkoa wa Shinyanga ni Hassan Mwendapole, Mbala Mlolwa na Erasto Kwilasa.

Kwa mkoa wa Singida, wagombea wa nafasi hiyo ni Hanje Barnabas, Misanga Hamis, Martha Mlata na Kilimba Juma.

Wagombea wa halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa Nyamagana ni Dk Sillinus Nyanda, Jamal Babu, Kelebe Lutelil na Patrick Nyabugongwe.

Wagombea wa nafasi hiyo wilaya ya Kahama ni Pili Izengo, Paschal Mayengo na Sweetbert Nkuba huku Monduli ikiwa na mgombea mmoja, Namelock Sokoine.

Wagombea uenyeviti CCM wilaya ya Monduli ni Loata Sanare huku Sumbangawa mjini ikiwa na wagombea wawili, Chami Mask na Godfrey Mwikala.

Nafasi ya katibu wa uchumi na fedha Mkoa wa Kilimanjaro inagombewa na Shadrack Amani, Chata Joseph na Karia Mahamoud.

Wanaogombea nafasi ya katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Arusha ni Semmy Kiondo, Shaaban Mdoe na Veraikunda Urio.

Wanaogombea nafasi ya uenyeviti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha ni Eric Edward, Lengai Thomas na Mwanzani Omar.

Kwa mkoa wa Shinyanga wanaowania nafasi hiyo ni Mabembela Elias, Mipanda Dalushi, Ndasa Damian na Shigela Bernard.

Credits: Mwananchi






ZeroDegree.
CCM kujaza nafasi za waliotimkia Ukawa CCM kujaza nafasi za waliotimkia Ukawa Reviewed by Zero Degree on 2/09/2016 10:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.