Loading...

Hali ya Mufti Abubakar Zuberi yaimarika.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakimfariji Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.



Dar es Salaam. Hali ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuberi ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu inaendelea vizuri.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Mwangomo alisema mufti amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

“Uamuzi wa kutaja ugonjwa unaomsumbua ni wa mufti mwenyewe, ninachoweza kusema leo (jana) anaendelea vizuri,” alisema.

Alisema mufti amelazwa katika chumba ambacho wanaruhusiwa kuingia watu maalumu wanaompelekea chakula.

Baadhi ya waumini wa Kiislamu jana mchana walionekana nje ya jengo hilo wakitaka kufahamu maendeleo ya afya ya kiongozi wao huyo.

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Suleiman Lolila alipotakiwa kuzungumzia hali ya mufti alisema yuko hospitali na mgonjwa na kukata simu. Sheikh Khamis Mataka ambaye ni Katibu mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni Tanzania, aliwataka waislamu kumwombea kiongozi huyo ili apone haraka na kuendelea na majukumu yake.





ZeroDegree.
Hali ya Mufti Abubakar Zuberi yaimarika. Hali ya Mufti Abubakar Zuberi yaimarika. Reviewed by Zero Degree on 2/09/2016 10:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.