Loading...

JIPU ndani ya IKULU....??? Soma hapa lawama za wasanii wa sanaa za uchoraji walizoitupiua serikali.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelaumiwa na wasanii wa sanaa za uchoraji, mara baada ya wasanii hao kudai kuwa serikali hiyo haijawalipa ujira wao baada ya kazi za uchoraji picha za asili ndani ya ikulu hiyo.



Wakizungumza na Mtembezi.com wasanii hao wamesema walipata tenda ya uchoraji michoro ya utamaduni ndani ya ikulu hiyo iliyopo Magogoni jiini Dar es salaam.



Mmoja wa wasanii hao wa sanaa za uchoraji anae fahamika kwa jina la Masoud Kibwana amesema ameeleza malalamiko juu ya ucheleweshwaji wa malipo ya ya kazi zao za sanaa, ambazo zilichukuliwa kwa ajiri ya mapambo ndani ya Ikulu hiyo ambapo amesema kazi hizo zilikusanywa tangu mwaka jana mwezi wa 8 ikiwa ndani ya kipindi cha kampeni ambapo waliambiwa kuwa watalipwa pesa zao kabla ya kipindi hicho kuisha.



Aidha amesema wame shangazwa na hatua ya serikali kuwa cheleweshea fedha zao licha ya muda mrefu kupita kinyume na makubaliano yao.


Vilevile ameeleza kuwa kiongozi ambae alikuwa ameshika tenda hiyo ambae amemtaja kwa jina la George Bakelana hapatikani kwenye simu na hata akipatikana hapokei simu zao na baada ya siku kadhaa kupita kiongozi huyo aliwapigia simu na kuwaambia kuwa atawapa maelekezo juu ya kazi zao.

Akieleza baadhi ya hatua walizozipitia kutatua suala hilo msanii huyo wa sanaa ya uchoraji amesema wamejitahidi kufanya ufuatiiaji kupitia Shirikisho la Sanaa Tanzania bila mafanikio yeyote.

Source: Mtembezi.



ZeroDegree.
JIPU ndani ya IKULU....??? Soma hapa lawama za wasanii wa sanaa za uchoraji walizoitupiua serikali. JIPU ndani ya IKULU....???  Soma hapa lawama za wasanii wa sanaa za uchoraji walizoitupiua serikali. Reviewed by Zero Degree on 2/25/2016 03:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.