Loading...

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya [ CHADEMA ] akamatwa na polisi akiwa hotelini jijini Mwanza.


Mbunge wa jimbo la Bunda, Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza usiku wa kuamikia leo na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.

Wabunge hawa pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA Wako jijini Mwanza kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest.




ZeroDegree.
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya [ CHADEMA ] akamatwa na polisi akiwa hotelini jijini Mwanza. Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya [ CHADEMA ] akamatwa na polisi akiwa hotelini jijini Mwanza. Reviewed by Zero Degree on 3/12/2016 10:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.