Loading...

China imekana kuhusika na uuzaji wa nyama za binadamu Barani Afrika.


Wizara ya masuala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng’ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China akisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.

Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina ukweli wowote huku Balozi wa China nchini Zambia, Yang Youming akisema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili.

”Leo jarida moja linasambaza uvumi, likidai China inatumia nyama ya binadamu ambayo huihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika.Hii ni dhuluma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi”.

Source: Mtembezi




ZeroDegree.
China imekana kuhusika na uuzaji wa nyama za binadamu Barani Afrika. China imekana kuhusika na uuzaji wa nyama za binadamu Barani Afrika. Reviewed by Zero Degree on 5/24/2016 10:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.