Loading...

Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu AKANUSHA kupinga sakata la UTUMBUAJI majipu.


Samia Hassan Suluhu

Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu amewataka Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya, kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma wanapotaka kufukuza kazi watumishi wanaokwenda kinyume. 

Samia alisisitiza kuwa hajawahi kupinga utumbuaji majipu kama ambavyo alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Hata hivyo, aliwaambia wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kwamba mwenye mamlaka ya kutumbua majipu ni Rais pekee, kwa kuwa anateua, anaajiri na kufukuza. Alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha juu ya agizo lake la kutaka mifugo iliyo ndani ya hifadhi za Taifa (Tanapa) ihamishwe.


Samia Hassan Suluhu

Alisema Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini, wanapaswa kuhakikisha wanapotaka kuwawajibisha watumishi wa umma wanafuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

“Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuteua, kutengua na kuajiri; lakini sijapinga utumbuaji wa majipu bali nasisitiza kila RC (Mkuu wa Mkoa) na DC (Mkuu wa Wilaya) afuate sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” alisema mama Samia huku akisisitiza mifugo inayotoka nje ya nchi iliyomo kwenye hifadhi za taifa, kuhakikisha inaondolewa ifikapo Juni 30.




ZeroDegree.
Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu AKANUSHA kupinga sakata la UTUMBUAJI majipu. Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu AKANUSHA kupinga sakata la UTUMBUAJI majipu. Reviewed by Zero Degree on 5/19/2016 10:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.