RUMBESA zapigwa marufuku kutumika katika uuzwaji wa mazao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim amesema kitendo cha wanunuzi wa mazao kushindilia magunia na kushonea magunia kama kichuguu maarufu kama rumbesa huko ni kuwaibia wakulima na kukiuka sheria.
Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CUF) Saumu Sakala juu ya kauli ya serikali kwa wafanyabishara wanaofunga rumbesa na kuikosesha serikali mapato na kuwanyonya wakulima.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema ni kweli wapo wafanyabiashara wanaonunua mazao kwa rumbesa na serikali ilishatoa maagizo kuhusiana na jambo hilo na kuonekana kukiukwa, Majaliwa akaagiza Wakala wa Vipimo nchini kuhakikisha jambo hilo linafanyiwa kazi na kuhakikisha magunia yanapimwa vijijini kuhakikisha yanajazwa katika ujazo wake wa kawaida na si rumbesa.
Aidha Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kwa kuwa wao ni wakuu wa ulinzi na usalama katika maeneo yao kuhakikisha wanashiriki kukomesha jambo hilo ili serikali iweze kupata mapato na wakulima waweze kunufaika na mazao yao.
ZeroDegree.
RUMBESA zapigwa marufuku kutumika katika uuzwaji wa mazao.
Reviewed by Zero Degree
on
5/20/2016 10:23:00 AM
Rating: