Loading...

Serengeti boys kucheza na Malaysia leo.



Serengeti Boys

Timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’inashuka dimbani leo kuchuana na Malaysia.

Mchezo huu utapigwa katika uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa India ikiwa ni mchezo wa kuwania nafasi ya tatu kwenye michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Katika mchezo wa kuwania kucheza fainali, Serengeti Boys iliruhusu sare ya mabao 2-2 Malaysia hivyo kufikisha sare ya tatu baada ya kushinda mechi moja.

Serengeti Boys imemaliza hatua ya awali ikiwa na pointi sita sawa na Korea Kusini, lakini ikazidiwa bao moja hivyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ambayo Marekani iliongoza kwa kufikisha alama nane.

India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.



ZeroDegree.
Serengeti boys kucheza na Malaysia leo. Serengeti boys kucheza na Malaysia leo. Reviewed by Zero Degree on 5/25/2016 02:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.