Loading...

Wahukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kujaribu kushambulia ndege.


Mahakama ya kijeshi mji mkuu wa Somalia Mogadishu, imewahukumu kifungo cha maisha wanaume wawili ambao walipatikana na hatia ya kupanga shambulizi dhidi ya ndege ya shirika la Daallo mwezi Februari.

Bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu ikiwa safarini kwenda nchini Djibouti.

Shimo lilitobolewa kando mwa ndege hiyo lakini hata hivyo ndege haikusambaratika.



Abiria mmoja ambaye alitupwa nje ya ndege hiyo aliaga dunia na wengine wawili wakajeruhiwa.

Washtakiwa wengine wanane walihukumiwa vifungo vya kati ya miezi sita na miaka minne.

Hao ni pamoja na waliokuwa wafanyikazi wa uwanja wa ndege na maafisa wa ulinzi.

Source: BBC




ZeroDegree.
Wahukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kujaribu kushambulia ndege. Wahukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kujaribu kushambulia ndege. Reviewed by Zero Degree on 5/30/2016 02:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.