Loading...

Wale WANAOIBEZA SerikaliI ya Magufuli wapewa Onyo.


Wanaharakati na wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, wametakiwa kuacha kuupotosha umma juu ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali hiyo chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa CZI – Information And Media Consults Co. Ltd, Augustino Matefu wakati wa mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha mafanikio makubwa katika sekta ya ukusanyaji mapato, elimu, miundombinu, afya na kujenga uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.

Hivyo alitoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano na kuwapuuza wanaharakati na wanasiasa hao wanaunga mkono wale wasioitakia mema Tanzania na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujumla.

Alisema katika sekta ya mapato, Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miezi saba iliyopita imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 900 kwa mwezi kabla ya utawala wake hadi shilingi trilioni 1.5 kwa sasa




ZeroDegree.
Wale WANAOIBEZA SerikaliI ya Magufuli wapewa Onyo. Wale WANAOIBEZA SerikaliI ya Magufuli wapewa Onyo. Reviewed by Zero Degree on 5/20/2016 09:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.