Loading...

AJALI: Watu 6 wafariki papo hapo baada ya basi dogo kugongana uso kwa uso na Lori wilayani Same.


Same/Moshi. Watu sita wamefariki dunia papo hapo, baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na Lori katika eneo la Sababa wilayani Same barabara kuu ya Moshi-Dar.

Mashuhuda wa ajali hiyo mbaya iliyotokea usiku kuamkia leo wakiwamo majeruhi, walimtupia lawama dereva wa basi ambaye naye ni miongoni mwa waliokufa, kwamba licha ya kunukia pombe lakini alikuwa na mwendo kasi. 

Ajali hiyo ilitokea saa 1:30 usiku na kusababisha vifo hivyo na majeruhi tisa na kwamba basi hilo lilikuwa likitokea Same Mjini kuelekea Kijiji cha Njoro kabla ya kugongana uso kwa uso na lori.

Koka Moita

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Koka Moita amewataja waliofariki dunia kuwa Eliakim Robert (35) Samson Rialamu (48) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Thomas (25). Alisema watu watatu bado hawajatambuliwa.

ZeroDegree.
AJALI: Watu 6 wafariki papo hapo baada ya basi dogo kugongana uso kwa uso na Lori wilayani Same. AJALI: Watu 6 wafariki papo hapo baada ya basi dogo kugongana uso kwa uso na Lori wilayani Same. Reviewed by Zero Degree on 6/11/2016 06:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.