Loading...

UNESCO kutoa MAFUNZO kuhusu TSUNAMI kwa Watanzania.


Watanzania wapata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu Tsunami Kutokanana kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa,
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.


Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCOnchini, Zulmira Rodrigues.

Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCOnchini, Zulmira Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja namadhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine.



“Watu wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa,” alisema Bi. Rodrigues.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.Leonard Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na kusababisha vifo vya waogeleaji watano.

“Mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali,” alisema Dk. Chamuriho.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
UNESCO kutoa MAFUNZO kuhusu TSUNAMI kwa Watanzania. UNESCO kutoa MAFUNZO kuhusu TSUNAMI kwa Watanzania. Reviewed by Zero Degree on 6/21/2016 09:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.