Loading...

Aliyekuwa Kocha wa Nigeria Stephen Keshi Kuzikwa Julai 29.



MAZISHI ya aliyekuwa Kocha Mkuu na nahodha wa Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) Stephen Keshi, aliyefariki Juni 8 mwaka huu, yatafanyika Julai 29 nyumbani kwao mjini Illah, Oshimili Kaskazini, Jimbo la Delta.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Habari wa Delta, Patrick Ukah, ambaye ni mjumbe wa kamati ya mazishi ya Keshi, shughuli za mazishi hayo zitaanza Julai 28 na kumalizika Julay 31.

Pamoja na kuwepo na sala maalum katika Kanisa Katoliki na shughuli mbalimbali za maombi, patakuwepo pia na mechi ya soka itakayohusisha nyota mbalimbali nchini humo. ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa heshima maalum kwa marehemu ambaye aliwika katika soka.


Source: GPL
ZeroDegree.
Aliyekuwa Kocha wa Nigeria Stephen Keshi Kuzikwa Julai 29. Aliyekuwa Kocha wa Nigeria Stephen Keshi Kuzikwa Julai 29. Reviewed by Zero Degree on 7/21/2016 07:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.