Loading...

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga arejea jimboni Misungwi.


Charles Kitwanga

Mwanza. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amekutana na waandishi wa habari nyumbani kwake Misungwi leo akisema amerejea jimboni kufanya kazi ya kutumikia wapiga kura.

Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais John Magufuli kutokana na kuingia bungeni na kujibu swali akiwa amelewa, amesema sasa atakaa jimboni muda mrefu kuliko awali alipobanwa na shughuli nyingine ya uwaziri.

Tangu afukuzwe kazi, Kitwanga ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mwigulu Nchemba, hajaonekana hadharani wala kukutana na vyombo vya habari hadi hivi karibuni picha zake ziliposambazwa akikabidhi ofisi kwa Nchemba.

Kitwanga ni mbunge wa jimbo la Misungwi kupitia CCM.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga arejea jimboni Misungwi. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga arejea jimboni Misungwi. Reviewed by Zero Degree on 7/04/2016 12:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.