Loading...

Juan Mata kujiunga na Everton..?? Huu hapa ufafanuzi kuhusu tetesi hizo.


Licha ya Jumapili ya Juni, 3 vilabu vingi barani Ulaya kufanya usajili lakini pia zilisambaa habari na picha zikimwonesha kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Juan Mata akiwa na jezi ya Everton ikiwa na maelezo kuwa Mata amejiunga na klabu hiyo ya Everton.

Taarifa za Mata kujiunga Everto zilisambaa zaidi katika makundi ya WhatsApp na mashabiki wengi wa soka kuamini kuwa ni kweli mshambualiaji huyo rais wa Hispania amejiunga a Everton ambayo imepata meneja mpya, Ronald Koeman.

Lakini jambo hilo halina uhalisia na kimechofanyika ni kupotosha mashabiki wa soka na uhalisia ni kwamba Everton inahitaji kumsajili Mata kwa kitita cha Pauni Milioni 20 lakini bado hawajafikia makubaliano yoyote na Manchester United.

Kama Man United ikimuachia Mata basi moja kwa moja kocha mpya wa United, Jose Mourinho anaweza kutajwa kuwa sababu kubwa ya kiungo huyo kuondoka kwani hata wakati akiifundisha Chelsea alimuuza mchezaji huyo kwa sababu kuwa haendani na kasi yake.

Pamoja na Mourinho kuhusishwa na kumuondoa Mata mwingine anayetajwa ni kiungo mshambualiaji wa Dortmund, Henrikh Mkhitaryan ambaye anacheza nafasi moja na Mata na ikiwa tayari ameshadhibitishwa kujiunga Man United na sasa akisubiri kufanyiwa vipimo hivyo kuchangia Mata kuwa rahisi kuondoka Man United.


ZeroDegree.
Juan Mata kujiunga na Everton..?? Huu hapa ufafanuzi kuhusu tetesi hizo. Juan Mata kujiunga na Everton..?? Huu hapa ufafanuzi kuhusu tetesi hizo. Reviewed by Zero Degree on 7/04/2016 10:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.