Loading...

Madawati mapya zaidi ya 500,000 yamepatikana kwa NJIA YA UCHANGIAJI.


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kampeni ya kuhamasisha wadau kuchangia madawati imezaa matunda na kufanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la madawati katika shule za msingi na sekondari.

Akihitimisha mkutano wa tatu wa bunge la 11, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani na kuhamasisha uchangiaji kutoka kwa wadau mbalimbali, jumla ya madawati 552,630 yamepatikana hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu.


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Amesema madawati hayo yaliyopatikana yamefanya jumla ya madawati yaliyopo hadi sasa katika shule za msingi na sekondari kufikia 2,672,397 sawa na asilimia 77 ya mahitaji ya madawati yaliyopo.

Amesema upungufu uliopo hadi sasa ni madawati 792,949 sawa na asilimia 23, na kuagiza wakuu wa mikoa na wilaya kushughulikia upungufu huo mara moja kama ambavyo Rais Magufuli aliagiza.

Amesema kwa upande wa shule za sekondari, hadi sasa kuna jumla ya madawati 1,397,138 sawa na asilimia 93 ya mahitaji na kuna upungufu wa madawati 112,885 sawa na asilimia 7%.


ZeroDegree.
Madawati mapya zaidi ya 500,000 yamepatikana kwa NJIA YA UCHANGIAJI. Madawati mapya zaidi ya 500,000 yamepatikana kwa NJIA YA UCHANGIAJI. Reviewed by Zero Degree on 7/01/2016 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.