Loading...

Ndoto za soka za Adam Johnson zatokomea gizani [ Soma hapa kujua yaliyomkuta nyota huyo ].

Kila mwanadamu mwenye akili timamu huwa na ndoto zake ambazo anatamani kuzifikia japo kuwa
njia tunazopita hufanya ndoto hizi kupata changamoto au wakati mwingine kutotimia kabisa. Mipango madhubuti na nidhamu ndiyo ngao ya kufikia ndoto zako.

Mwaka 2005 katika Ligi Kuu ya England vyombo vya habari vilikuwa vikimtaja kijana mdogo ambaye alikuwa ni “Promising Talent” huyu ni Adam Johnson. Klabu ya Middlesbrough ndiyo iliyomlea kijana huyu hadi akawa lulu kiasi kwamba vilabu vikubwa vikimgombania.

Hatimaye mwaka 2010 matajiri wa Manchester City wakafanikiwa kumnasa na kumlipa mshahara mnono kabisa lakini alishindwa kuhakikishiwa nafasi kikosini kwa sababu ya uwepo wa nyota wengi klabuni hapo alicheza mechi 7.

Baada ya mambo kuwa magumu Johnson alijiunga na Klabu ya Sunderland ambayo ilionekana ni sehemu salama kwake lakini mwaka 2014 alikumbwa na hatia ya kufanya mapenzi na binti wa miaka 15 wakati ambao mchumba wake alikuwa mjamzito.



Hapa ndipo ndoto za soka la Johnson zilipoyumba. Hivi sasa amehukumiwa kifungo cha miaka sita lakini tayari Sunderland imevunja mkataba wake, Adidas pia wamevunja nae mkataba, na hata mkataba wa game ya FIFA 2016 umevunjwa.

Ndoto zimetokomea gizani, pole Adam Johnson lakini kwa leo hongera Kwa kuongeza mwaka mwingine wa kuishi.



ZeroDegree.
Ndoto za soka za Adam Johnson zatokomea gizani [ Soma hapa kujua yaliyomkuta nyota huyo ]. Ndoto za soka za Adam Johnson zatokomea gizani [ Soma hapa kujua yaliyomkuta nyota huyo ]. Reviewed by Zero Degree on 7/20/2016 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.