Loading...

Rais Magafuli atengua uteuzi wa Mwenyeketi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Dk James Wanyancha.

RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Dk James Wanyancha.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi iliyotolewa mjini Dodoma jana ilisema Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia Julai 28, 2016.

Ilisema kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Balozi Kijazi, uteuzi wa Haule ulianza jana Julai 28. Kabla ya uteuzi huo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara.

Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.

ZeroDegree.
Rais Magafuli atengua uteuzi wa Mwenyeketi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara. Rais Magafuli atengua uteuzi wa Mwenyeketi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara. Reviewed by Zero Degree on 7/29/2016 09:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.