Loading...

TANZIA: Mchekeshaji Ismail Issa Mapembe [ Mjomba Kundambanda ] afariki dunia.

Limekuwa pigo jingine kwa tasnia ya filamu nchini Tanzania hususani kwa upande wa uchekeshaji mara baada
ya taarifa za kifo cha msanii Kundambanda kusambaa mitandaoni siku hii ya leo baada ya wasanii wenzake kupost picha zake na kuelezea kuwa hatunae tena duniani.

Mchekeshaji huyo aliyekuwa maarufu Zaidi kwa jina la Mjomba Kundambanda au Baba Kundambanda alipendelea Zaidi kucheza kama askari katika filamu mbalimbali alizokuwa akishiriki.

Mapembe alijipatia umaarufu kupitia maigizo ya televisheni ‘Vituko Show’ yaliyokuwa yakioneshwa Channel Ten na litakuwa pigo kubwa kutokana na wasanii wachache kucheza kipengele alichokuwa akikimudu vizuri mbele ya kamera.

Taarifa za awali zinasema kuwa Mjomba Kundambanda alifariki akiwa nyumbani kwao Masasi huko mkoani Mtwara na sababu zilizopelekea kupoteza maisha msanii huyo bado hazijajulikana.

Wasanii waliomuenzi muigizaji huyo kwa kupost picha katika mitandao ya kijamii ni pamoja na Mkudesimba (Kitale), Daudi Michael, Mkwere Orijino, Stan Bakora na wengine wengi wa Bongo Movie.



ZeroDegree.
TANZIA: Mchekeshaji Ismail Issa Mapembe [ Mjomba Kundambanda ] afariki dunia. TANZIA: Mchekeshaji Ismail Issa Mapembe [ Mjomba Kundambanda ] afariki dunia. Reviewed by Zero Degree on 7/22/2016 07:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.