Loading...

Ureno yabeba ubingwa wa EURO 2016.

Ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda Euro.

Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris.

Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kusababisha huzuni kubwa kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France

Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa.

Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.

Eder asherehekea na wenzake baada ya kufunga.

Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.


ZeroDegree.
Ureno yabeba ubingwa wa EURO 2016. Ureno yabeba ubingwa wa EURO 2016. Reviewed by Zero Degree on 7/11/2016 09:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.