Loading...

Wanaharakati wataka Koffi Olomide ashtakiwe DRC.

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kimemokrasia ya Congo, liitwalo Asvoko, limeiomba serikali ya nchi hiyo kumfungulia mashataka mwanamuziki Koffi Olomide.

Hii ni baada ya kuonekana katika video iliyosambaa mitandaoni akimpiga teke mmoja wanamuziki wake wa kike kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi ijumaa wiki iliopita.

Wakati huo huo shirika la Zambia la kilimo na biashara limefutilia mbali tamasha ambalo Koffi alipanga kulifanya nchini humo.

Kutoka Goma, Byobe Malenga ametuandalia taarifa hii.

Source: BBC
ZeroDegree.
Wanaharakati wataka Koffi Olomide ashtakiwe DRC. Wanaharakati wataka Koffi Olomide ashtakiwe DRC. Reviewed by Zero Degree on 7/25/2016 06:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.