Loading...

Zaidi ya ombaomba 50 wakamatwa Jijini Dar.

Jumla ya ombaomba sitini (60) wamekamatwa katika msako wa ombaomba unaoendelea katika jiji la Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe alipokuwa akitoa majibu ya uwepo wa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam licha ya kuwepo kwa operesheni ya kuwaondoa.


Akifafanua Dkt. Magembe amesema Zoezi la ukamataji wa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam linaendelea na ombaomba sitini wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka, wakiwemo watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao wamepelekwa katika vituo vya watoto yatima kikiwemo kituo cha Kurasini.

Dkt. Magembe alisema kuwa bado ombaomba wamekuwa wakionekana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kuwepo kwa watu wanaotoka mikoani na kuingia katika makundi ya ombaomba kila siku.


Aidha, amesema kuwa kutokana na kuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaotoka mikoani na kujiingiza katika makundi ya ombaomba, uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam unashirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoa elimu mikoani juu ya operesheni ya kuondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam wanaosababishwa na watu wanaokuja kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.


ZeroDegree.
Zaidi ya ombaomba 50 wakamatwa Jijini Dar. Zaidi ya ombaomba 50 wakamatwa Jijini Dar. Reviewed by Zero Degree on 7/15/2016 10:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.