Loading...

Zaidi ya Simu milioni 10 za Android zaathiriwa na kirusi.

Hadi simu milioni 10 aina ya Android zimeambukizwa virusi vinavyotoa Clicks bandia kwa ajili ya matangazo kulingana na watafiti.

Kirusi kinachoathiri simu za Android.

Programu hiyo pia inaweka apps na kumchunguza mwenye akaunti.

Kirusi hicho kinawapatia takriban dola 300,000 kila mwezi waliokianzisha.

Simu nyingi ambazo zimeathiriwa na kirusi hicho zipo nchini China

Ongezeko la simu zilizoathiriwa na kirusi hicho lilibainika na kampuni ya usalama wa mitandao Checkpoint na Lookout.

Kirusi hicho kinatoka familia ya Shedun by Lookout but Hummingbad by Checkpoint.

Smartphone

Asilimia kubwa ya simu zilizoathiriwa na virusi hivyo zipo nchini China na ziligunduliwa na kampuni mbili tofauti za masuala ya mitandaoni ya Checkpoint na Lookout.

Virusi hivyo vinafahamika kwa jina la Himmingbad na hujipati uwezo wa kuindesha simu yako na kuutuma kwa wavumbuzi ambao sasa wataweza kuindesha simu yako kwa kurusha matangazo yao na kuweka programu zao kwenye simu yako

Hata unapofuta kila kitu ndani ya simu yako, kirusi hicho kinaweza kujificha kisitoka na husumbua sana unapojaribu kukiondoa (uninstall).

Katika blogu,Checkpoint imesema kuwa imefanikiwa kubaini kithibiti cha simu zilizoathiriwa ambacho kinaonyesha kuwa Hummingbad imeathiri simu milioni 10.

China ,India,Ufilipino na Indonesia zinaongoza katika mataifa yenye simu zilizoathirika.


ZeroDegree.
Zaidi ya Simu milioni 10 za Android zaathiriwa na kirusi. Zaidi ya Simu milioni 10 za Android zaathiriwa na kirusi. Reviewed by Zero Degree on 7/10/2016 10:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.