Loading...

Asiyevaa HELMENTI kufungwa jela miezi 6 au kulipa faini ya shilingi laki 3.

BIASHARA ya Bodaboda imeshamiri katika Jiji la Dar es Salaam lenye wakazi zaidi ya milioni nne. Hata hivyo, licha ya ukweli kwamba helmeti kupunguza kwa asilimia 69 hatari ya mwendesha pikipiki kuumia kichwa pale apatapo ajali, na kapunguza kifo kwa asilimia 42, uvaaji wa helmeti kwa madereva na abiria wao bado ni kitendawili.


Kamanda wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Awadhi Haji anasema wameshatoa elimu ya kutosha kwa waendesha pikipiki ili wahakikishe wanavaa kofia ngumu pamoja na abiria wao wakati wanapopanda pikipiki.

“Watakaokaidi agizo tutawakamata madereva na abiria wao na kuwafikisha mahakamani. Huko wanaweza kutozwa faini inayoanzia Sh 300,000 au kufungwa jela kati ya miezi sita au mwaka mmoja kutokana na sheria ya Sumatra,” anasema kamanda Haji.

Polisi wameamua kufanya hivyo kutokana na faini ya Sh 30,000 chini ya sheria ya usalama barabarani kutowaogopesha madereva wengi wa pikipiki. Ndiyo maana sasa uamuzi ni kuwapeleka mahakamani.

“Huko tunawashitaki chini ya sheria ya Sumatra na operesheni hii tunaifanya kwa kushirikiana na Sumatra wenyewe,” anasema ACP Haji.

Credits: Mtembezi
ZeroDegree.
Asiyevaa HELMENTI kufungwa jela miezi 6 au kulipa faini ya shilingi laki 3. Asiyevaa HELMENTI kufungwa jela miezi 6 au kulipa faini ya shilingi laki 3. Reviewed by Zero Degree on 8/04/2016 09:21:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.