Loading...

Mavugo afungua tawi jipya la Simba Nchini Burundi.

BAADA ya kujiunga na Simba, straika wa kimataifa wa timu hiyo, Laudit Mavugo, amekuwa gumzo nchini kwao Burundi ambapo idadi kubwa ya marafiki na ndugu zake wamekuwa wakimwomba awatumie jezi za Wekundu hao wa Msimbazi jambo linalotafsiriwa kama amefungua tawi nchini humo.

Straika huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu, amewaambia wandishi wa habari kuwa tangu kutua hapa nchini amekuwa akipokea simu nyingi kutoka Burundi marafiki zake wakimtaka kuwatumia jezi za Simba.

“Tangu nitue hapa Tanzania marafiki zangu wengi wamekuwa wakinipigia simu niwatumie jezi za kutosha za Simba hasa namba tisa ambayo ninaitumia, wamekuwa wakinipa sapoti kubwa sana.

“Nadhani nitafanya kama wanavyotaka kwani mtu akikupa ushirikiano inatakiwa hata wewe umthamini ili kuzidi kujenga urafiki ulio imara,” alisema.


Credits: Dimba
ZeroDegree.
Mavugo afungua tawi jipya la Simba Nchini Burundi. Mavugo afungua tawi jipya la Simba Nchini Burundi. Reviewed by Zero Degree on 8/22/2016 11:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.