Loading...

Klabu ya Chelsea yanasa beki mpya toka Fiorentina ya Italia.

Chelsea wamethibitisha kumsajili beki Marcos Alonso kutoka Fiorentina ya Italy kwa ada ya paundi mil 23.

Alonso hatakuwa mgeni kwenye Ligi ya England baada ya hapo awali kuwahi kucheza katika vilabu vya Bolton na Sunderland.

Picha: Marcos Alonso, beki aliyesajiliwa na klabu ya Chelsea ya Uingereza.
Usajili huo hauishii hapo kwa Chelsea kwani bado wanahusishwa na mipango ya kumrejesha beki wao wa zamani David Luiz kwa ada ya paundi mil 32 ambaye miaka miwili iliyopita walimuuza kwenda PSG kwa ada ya paundi mil 50.

Wakati huo huo, winga wao Juan Cuadrado amerudi tena Juventus kwa mkopo wa msimu mzima.


Credits: ShaffihDauda
ZeroDegree.
Klabu ya Chelsea yanasa beki mpya toka Fiorentina ya Italia. Klabu ya Chelsea yanasa beki mpya toka Fiorentina ya Italia. Reviewed by Zero Degree on 8/31/2016 08:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.