Loading...

Kiongozi wa kikundi cha Islamic State [ IS ] auawa kwa shambulizi lililofanywa na Jeshi la Misri.

Mtu mmoja anayetajwa kuwa kiongozi wa kikundi cha Islamic State (IS), Abu Duaa al-Ansari ameuwawa pamoja na wanajeshi wenzake wa IS 45 na jeshi la Misri baada ya kufanyika shambulizi la anga.

Abu Duaa al-Ansari ambaye alikuwa ni kiongozi wa IS katika eneo la Sinai, alikutwa tukio hilo katika mji wa El-Arish kipindi ambacho jeshi la Misri limekuwa likifanya operesheni kwa katika maeneo ya Sinai na Cairo.

Katika taarifa aliyotolewa na jeshi la Misri ilisema kuwa tukio hilo lilitekelezwa kwa umakini ili kuhakikisha wanawashambulia wanajeshi la IS.

Kundi hilo la IS liliweka kambi katika eneo la Sinai tangu mwaka 2011 na mpaka sasa hawajatoa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo.

ZeroDegree.
Kiongozi wa kikundi cha Islamic State [ IS ] auawa kwa shambulizi lililofanywa na Jeshi la Misri. Kiongozi wa kikundi cha Islamic State [ IS ] auawa kwa shambulizi lililofanywa na Jeshi la Misri. Reviewed by Zero Degree on 8/05/2016 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.