Loading...

Maji yaweka rehani ndoa za watu.

Ndoa za wakazi wa vijiji vya Nyamilihango, Bugulula na Isabilo Mkoani Geita, zimeelezwa kuwa hatarini kuvunjika kutokana na wanawake kutumia muda wa usiku kutafuta huduma ya maji.

Diwani wa Viti Maalumu (CCM), Kata ya Bugulula, Dorothea Ernest amesema hayo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi kutembelea eneo hilo kujua changamoto zinazowakabili.

Amesema akinamama wanaamka saa tisa usiku kuwahi kisimani kuweka foleni ya maji kutokana na vijiji hivyo kukabiliwa na ukosefu wa huduma hiyo.




Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Maji yaweka rehani ndoa za watu. Maji yaweka rehani ndoa za watu. Reviewed by Zero Degree on 8/17/2016 11:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.