Loading...

Manji ajiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa Yanga, ....serikali yatajwa kuhusika.

Taarifa ambazo zimezagaa muda mfupi kutoka kwa chanzo cha ndani cha klabu ya Yanga zinaeleza kuwa klabu hiyo imepata mshtuko baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa klabu hiyo.




Katika taarifa ambayo imewekwa mtandaoni na mmoja wa wanachama wa Yanga ambaye yupo karibu na uongozi, Godlisten Anderson ameandika katika akaunti yake ya Instagram na Facebook kuwa Manji amejiuzulu kuingoza Yanga kwa madai ya kupata shutuma kutoka kwa viongozi wa serikali na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanatumiwa na wafanyabiashara ambao hawana nia njema na Yanga.

Aidha sambamba na kujiuzulu nafasi hiyo, pia inaelezwa kuwa Manji amesitisha mpango wake wa kuitumia Yanga kibiashara kwa kuikodisha na kutumia nembo ya Yanga kwa miaka 10.

Hilo linaelezwa kuwa pigo kubwa ndani ya Yanga kwani tayari wapinzani wao Simba wapo katika hatua za kufanya mabadiliko na hilo linatajwa kuwachanganya viongozi wa Yanga kwani inasemekana kuwa wamekuwa wakipishana katika ofisi za Manji zilizopo katika jengo la Quality Plaza.

Aidha Mo Blog ilipojaribu kumtafuta Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ili azungumzie taarifa hizo simu yake iliita bila kupokelewa.




Source: Dewijblog
ZeroDegree.
Manji ajiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa Yanga, ....serikali yatajwa kuhusika. Manji ajiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa Yanga, ....serikali yatajwa kuhusika. Reviewed by Zero Degree on 8/15/2016 09:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.