Loading...

Mmarekani aliyedanganya kuwa ni mzee akamatwa, ...akutwa na bunduki 2 na zaidi ya dola 25,000 pesa taslimu.

Shaun "Shizz" Miller amekuwa mafichoni tangu mwezi Aprili:

Polisi nchini Marekani wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja baada ya kugundua kuwa alikuwa akidanganya kuwa yeye ni mtu mzee.


Polisi walizingira nyumba moja huko Massachusetts na kumuamrisha Shaun "Shizz" Miller atoke nje.

Kisha akatoka nje akiwa amejibadilisha na kuwa kama mtu mzee, lakini baada ya uchunguzi wa kina polisi waligundua kuwa alikuwa ni mtuhumiwa waliyekuwa wakimtafuta mwenye umri wa miaka 31 na ndipo walipoamua kumkamata.

Amekuwa mafichoni tangu ashtakiwe kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya mwezi Aprili.

Wakati huo huo polisi waliendelea na msako zaidi ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kupata bunduki mbili na karibu dola elfu 30 pesa taslimu.


Creditd: BBC Swahili
ZeroDegree.
Mmarekani aliyedanganya kuwa ni mzee akamatwa, ...akutwa na bunduki 2 na zaidi ya dola 25,000 pesa taslimu.  Mmarekani aliyedanganya kuwa ni mzee akamatwa, ...akutwa na bunduki 2 na zaidi ya dola 25,000 pesa taslimu. Reviewed by Zero Degree on 8/21/2016 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.