Loading...

Mavugo ajisalimisha Simba.

SIMBA inazidi kunoga aisee. Baada ya wanachama kwa kauli moja kupitisha mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu yao ambao unawaruhusu wafanyabiashara kuwekeza hisa zao, sasa sikia hii, Laudit Mavugo yupo njiani anakuja.

Unajua ikoje! Mshambuliaji huyo Mrundi ambaye Simba walimfukuzia kwa muda mrefu aliamua kwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya majaribio ambapo amefeli na sasa amelitamkia DIMBA Jumatano kwa mdomo wake kuwa anakuja nchini.

Kwa sasa straika huyo ambaye anao uwezo mkubwa wa kupachika mabao yupo nchini kwao Burundi akiahidi kwamba muda wowote kuanzia sasa atatua kuungana na wenzake wa Simba waliopo chini ya Joseph Omog.

“Niko Burundi na siku yoyote kuanzia leo (jana) nitakuja Tanzania kujiunga na Simba, hivyo hapo nitakueleza kila kitu kuhusiana na safari yangu ya majaribio ya nchini Ufaransa.”

“Hii ni kweli kabisa nakuja Tanzania kujiunga na Simba, nadhani hata katika mchezo wao wa Simba Day nitakuwepo kilichobakia ni kumwomba Mungu,” alisema Mavugo.

Wakati Mavugo akisema hivyo, kwa upande mwingine rafiki wa straika huyo, Pierre Kwizera ambaye ni kiungo wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi alilithibitishia DIMBA Jumatano kuwa ni kweli Mavugo anakuja.

Kwizera ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Rayon Sport ya Rwanda alisema:

“Niko Burundi nimefika jana (juzi), hizo habari nimezisikia pia nimeonana na Mavugo, anakuja Tanzania muda wowote kwa ajili ya kujiunga na timu ya Simba,” alisema Kwizera.

Source: Dimba
ZeroDegree.
Mavugo ajisalimisha Simba. Mavugo ajisalimisha Simba. Reviewed by Zero Degree on 8/03/2016 09:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.