Loading...

Shibuda aifananisha UKAWA na Mlenda.

Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda amejitokeza katika mkutano wa Rais Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo anatatua kero za wananchi.


Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza Rais Dkt. Magufuli , Shibuda amevitaka vyama vingine vya siasa nchini kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya watanzania wote.

“Mheshimiwa Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa mlenda unamwangusha mtu mzima” – Amesema Shibuda.

Shibuda amesema vyama vya UKAWA vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni mtu mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa taifa.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Shibuda aifananisha UKAWA na Mlenda. Shibuda aifananisha UKAWA na Mlenda. Reviewed by Zero Degree on 8/12/2016 08:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.