Loading...

VIDEO: Tazama magoli aliyotupia Ibrahimovic jana Man U ilipoibuka kidedea dhidi ya Southampton kwa kuichakaza bao 3 kwa 1.

Usiku wa August 19 ilikuwa ni siku ambayo mashetani wa jiji la Manchester klabu ya Man United waliwakaribisha Southampton katika dimba lao la Old Trafford kucheza mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu England baada ya mchezo wao wa awali kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya AFC Bournemouth ugenini.

Mchezo dhidi ya Sothampton ulikuwa ni mchezo ambao ulitarajiwa kuangaliwa na mashabiki wengi zaidi duniani kutokana na kuwa hiyo ndio ilikuwa mechi ya kwanza yaPaul Pogba aliyevunja rekodi ya usajili ya dunia akitokea Juventus ya Italia na kurejeaMan United kwa pound zaidi ya milioni 100 baada ya kuondoka 2012.


Katika mchezo huo staa mwenye kujiamini zaidi kama ilivyo kwa kocha wake Zlatan Ibrahimovic, alifanikiwa kupachika magoli mawili yaliyoipa Man United point tatu na kufikisha jumla ya point sita katika msimamo wa EPL, Zlatan alianza kupachika goli la kwanza dakika ya 36 kisha akahitimisha kwa kufunga goli la pili dakika ya 52 kwa mkwaju wa penati.




ZeroDegree.
VIDEO: Tazama magoli aliyotupia Ibrahimovic jana Man U ilipoibuka kidedea dhidi ya Southampton kwa kuichakaza bao 3 kwa 1. VIDEO: Tazama magoli aliyotupia Ibrahimovic jana Man U ilipoibuka kidedea dhidi ya Southampton kwa kuichakaza bao 3 kwa 1. Reviewed by Zero Degree on 8/20/2016 09:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.