Loading...

VIDEO: Alichoongea Jose Mourinho baada ya aliyekuwa kocha wa Uingereza, Sam Allardayce kujiuzulu.

Imepita siku moja  toka aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Sam Allardayce atangaze kuachia nafasi yake hiyo kufuatia kugundulika kwa tuhuma nzito dhidi yake, Allardayce ametangaza kujiuzulu kufuatia uchunguzi wa gazeti la Telegraph kugundua kuwa alihusika kushauri uvunjifu wa sheria za usajili za FA.

Baada ya taarifa hizo kocha wa Man United, Jose Mourinho ameonesha kusikitika baada ya taarifa hizo kumfikia “Nachoweza kusema katika hili kiukweli namkubali Sam muda mrefu lakini nampa pole kwa kilichotokea kwa sababu amepoteza kazi ya ndoto yake kuifundisha timu ya taifa ya England, ninachoweza kusema kilichotekea hakiwezi kuvunja mahusiano yetu na yeye”

Aliyekuwa Kocha wa Timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce
Kama unakumbukumbu nzuri Sam Allardayce ameachia nafasi hiyo akiwa amedumu nayo kwa muda wa siku 67 tu tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, nafasi yake kwa sasa itashikwa na kocha wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Gareth Southgate wakati akitafutwa mbadala wake.


ZeroDegree.

VIDEO: Alichoongea Jose Mourinho baada ya aliyekuwa kocha wa Uingereza, Sam Allardayce kujiuzulu. VIDEO: Alichoongea Jose Mourinho baada ya aliyekuwa kocha wa Uingereza, Sam Allardayce kujiuzulu. Reviewed by Zero Degree on 9/29/2016 01:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.