Loading...

Bodi ya mikopo nchini yawaweka wanafunzi njia panda.

Wakati vyuo mbalimbali vikiwa vimefunguliwa nchini, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imewaweka njiapanda wanafunzi wanaostahili kupata mikopo kwa kuwa hadi jana orodha ya wanufaika ilikuwa haijatoka.

Hali hiyo ni tofauti na kilichoelezwa na bodi hiyo wiki iliyopita kwamba itahakikisha inatoa orodha hiyo kabla ya tarehe za vyuo kufunguliwa, lakini jana hali haikuwa hivyo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambacho kilifunguliwa tangu Jumamosi.

Baadhi ya wanafunzi wapya waliokuwa wameripoti UDSM wameanza usaili lakini wengi wameshindwa kukamilisha utaratibu huo kutokana na kutolipa ada. Idadi kubwa ya wanafunzi hao wanategemea mikopo kutoka HESLB.

Wakisubiri kukamilika kwa taratibu za mkopo ili kufahamu walionufaika na ambao hawatanufaika.

Bodi imetangaza utaratibu mpya wa mikopo katika mwaka wa masomo 2016/2017 ikisema kipaumbele ni kwa wanafunzi waliotoka kwenye kaya maskini, waliosoma shule za kata na waliotoka vijijini. Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Haki za Wanafunzi (TSNP), Shitindi Venance amesema hadi sasa wanafunzi wanaojiunga na masomo ambao wameomba mkopo walikuwa hawajui hatima yao.

ZeroDegree.
Bodi ya mikopo nchini yawaweka wanafunzi njia panda. Bodi ya mikopo nchini yawaweka wanafunzi njia panda. Reviewed by Zero Degree on 10/11/2016 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.