Loading...

Chelsea, Man City zafungasha virago kombe la ligi.

Manchester United walifika hatua ya robo fainali katika Kombe la EFL baada ya kuwalaza mabingwa watetezi Manchester City kwenye debi iliyochezewa uwanja wa Old Trafford.


Juan Mata alifunga bao la pekee mechi hiyo baada ya kupata mpira kutoka kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.

Paul Pogba alikuwa amegonga mlingoti kwa kombora kali awali na kusisimua mechi hiyo kipindi cha pili.

Kipindi cha kwanza kilikuwa kikavu bila upande wowote kupata kombora la kulenga goli.

Ushindi huo wa United ulikuwa wao wa pili katika mechi tano, na wa nne kwa Jose Mourinho katika mechi 18 alizokutana na Pep Guardiola.

Ulikuwa ni mwanzo mbaya kwa West Ham kutumia uwanja wa London.
West Ham nao wamefika hatua ya robo fainali Kombe la EFL baada ya kudhihirisha ubabe wao na kuwalaza Chelsea kwenye mechi iliyochezewa uwanja wa London, zamani ukijulikana kama uwanja wa Olimpiki.

Mechi hiyo hata hivyo ilikumbwa na vurugu za mashabiki.

Chupa za plastiki na viti vilirushwa mamia ya mashabiki walipokabiliana karibu na mwisho wa mechi.

Polisi wa kupambana na fujo walitumwa kudhibiti mashabiki.
Cheikhou Kouyate alifunga bao la kichwa kabla ya muda mapumziko, naye Edimilson Fernandes akaongeza la pili dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Gary Cahill alikomboa bao moja dakika za mwisho mwisho lakini lilikuwa tu la kufutia machozi.

Kwa ushindi huo, West Ham sasa watakutana na Manchester United.

John Terry alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu alipocheza dhidi ya Swansea tarehe 11 Septemba.
West Ham mechi yao ijao itakuwa dhidi ya Everton uwanjani Goodison Park ligini tarehe 30 Oktoba nao Chelsea siku hiyo wame ugenini St Marys dhidi ya Southampton.

Southampton nao walilaza Sunderland 1-0.

ZeroDegree.
Chelsea, Man City zafungasha virago kombe la ligi. Chelsea, Man City zafungasha virago kombe la ligi. Reviewed by Zero Degree on 10/27/2016 09:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.