Loading...

Jose Mourinho aanza visingizio vyake.

Mourinho amesema anahitaji kupewa muda zaidi ili kuitenengeza Manchester United na kuwa bora.

United wanakabiliwa na kibara kigumu mbele ya Stock City katika Uwanja wa Old Trafford Jumapili kabla ya kwenda mapumzikoni kupisha mechi za kimataifa na baadaye kurudi kukabiliana na Liverpool, Fenerbahce, Chelsea na Manchester City michezo hiyo ikichezwa ndani ya siku tisa

Na sasa akiwa tayari ameiongoza United kwenye michezo 10 tu, Mourinho amesema hatarajii kuwa amewajua kwa undani wachezaji wake pengine mpaka akae nao muda mrefu zaidi.


“Nahitahi muda. Nahitaji kuona wachezaji wangu wancheza, Nahitaji kuwaona wakiwa na utofauti mkubwa, Nihitaji kuwafahamu zaidi,” Mourinho aliwaambia wanahabari.

“Kuna mambo mengi sana ya kuangalia ili niwasome wachezaji wangu vizuri na hayo yote yatawezekna endapo nitakaa nao muda mzuri. Mara nyingi kuna utofauti kidogo unapokuwa umekaa na timu kwa miezi mitatu au minne na pengine mitano.”

ZeroDegree.
Jose Mourinho aanza visingizio vyake. Jose Mourinho aanza visingizio vyake. Reviewed by Zero Degree on 10/01/2016 06:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.