Loading...

Manchester yaichakaza Fenerbache goli 4 - 1 Europa Ligi.

Paul Pogba alifunga mara mbili wakati Manchester United walipoibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya klabu ya Fenerbahce katika kundi A.

Pogba mchezaji ghali zaidi duniani alifunga goli la kwanza kwa penalti baada ya Juan Mata kuangushwa ndani ya eneo la hatari, kisha baadaye kuandika bao la pili baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Jesse Lingard.

Bao la Robin Van Persie lilishangiliwa na mashabiki wa pande zote mbili.
Goli la Pili kwa United liliwekwa kimiani na Anton Martial kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku la mwisho likipachikwa na Jesse Lingard kwa shuti kali la chinichini.

Robin Van Persie aliiandikia timu yake ya Fenerbahce goli la kufutia machozi lililoshangiliwa na mashabiki wa pande zote akiwemo kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson.

ZeroDegree.
Manchester yaichakaza Fenerbache goli 4 - 1 Europa Ligi. Manchester yaichakaza Fenerbache goli 4 - 1 Europa Ligi. Reviewed by Zero Degree on 10/21/2016 10:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.