Loading...

Mbunge afafanua sakata la mishahara mitano hewa.

Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, amekanusha kiasi cha fedha kilichoingia kwenye akaunti yake kwamba si Sh23 milioni bali ni Sh5,091,734.96 ambazo zilikuwa hazieleweki.


Profesa Sigalla alitoa maelezo hayo jana alipofika ofisi za gazeti la mwananchi, baada ya kudaiwa kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano wakati alikwisha acha kazi hiyo alipoteuliwa kugombea ubunge wa Makete na kushinda.

Hali hiyo, iliyoelezwa kuisababishia Serikali hasara ya Shilingi 
milioni 23, ilitokana na madai kwamba hata baada ya kuacha kazi aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa Shilingi milioni 4.6 kutokana na ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Mbunge afafanua sakata la mishahara mitano hewa. Mbunge afafanua sakata la mishahara mitano hewa. Reviewed by Zero Degree on 10/19/2016 08:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.