Loading...

Tanesco wapewa miezi miwili kufikisha umeme kwa Bakhresa.

Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limepewa miezi miwili kuhakikisha inafikisha huduma ya umeme katika kiwanda cha kusindika matunda na kuzalisha juisi na vinywaji baridi cha Bakhresa Food Products Ltd kilichopo Mwandege wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.

Agizo hilo limetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda hicho iliyofanyika leo wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.

Amesema kuwa ni ajabu kwa mwekezaji kuanza ujenzi hadi anamaliza na baadaye anaanza uzalishaji halafu suala la nishati ya umeme linakuwa kikwazo hali inayomlazimu mwekezaji kutumia nishati mbadala (Jenereta) kitu kinachosababisha gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

“Ninaagiza hakikisheni mnafikisha umeme katika kiwanda hiki kabla ya mwezi wa 12, nia ajabu sana mtu anaanza kujenga mnamuangalia tu, anamaliza mnamuangalia, Meneja wa TANESCO upo? Hakikisha umeme unafika kama kuna mtu ana kukwamisha niambie”. Alisema Rais Magufuli.

Aliongeza ni imani yake kuwa baada ya umeme kufikishwa katika kiwaanda hicho gharama za undeshaji zitapungua na kupelekea kufanya maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wake.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametumia wasaa huo kumuomba Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa kuangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji kama huo katika maeneo mengine ya kikanda hili kutoa fursa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kupata soko la bidhaa zao.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Makampuni ya Bakhresa unasaidia kuchochea kilimo cha matunda na kutoa fursa ya soko la uhakika kwa wakulima.

Mwijage alisema kuwa Sekta ya Viwanda nchini imeendelea kukuwa, aliongeza kuwa adhima ya kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati kutokana na viwanda itatimia endapo wafanyabiashara wenye viwanda watakua wazalendo kama Bakhresa.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Bakhresa Food Production Ltd Bw. Yusuph Bakhresa ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara wenye viwanda nchini, hali ambayo itasaidia kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya kuitaka Tanzania kuwa nchi yenye viwanda ifikapo mwaka 2025.

ZeroDegree.
Tanesco wapewa miezi miwili kufikisha umeme kwa Bakhresa. Tanesco wapewa miezi miwili kufikisha umeme kwa Bakhresa. Reviewed by Zero Degree on 10/06/2016 05:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.