Loading...

TCRA imekifungia kipindi cha Take One cha Clouds Tv kwa muda wa miezi mitatu.

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Method Mapunda.
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia Kipindi chake cha Take One kwa muda wa miezi mitatu.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto. 

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.

Mahojiano yaliyopelekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00.

ZeroDegree.
TCRA imekifungia kipindi cha Take One cha Clouds Tv kwa muda wa miezi mitatu. TCRA imekifungia kipindi cha Take One cha Clouds Tv kwa muda wa miezi mitatu. Reviewed by Zero Degree on 10/04/2016 06:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.