Loading...

Vidonge vya maumivu chanzo cha ongezeko la vifo vya ghafla.

Dawa za maumivu zimetajwa kuwa chanzo cha ongezeko la vifo vya ghafla vitokanavyo na shambulio la moyo, utafiti uliochapishwa na jarida la kitabibu la Scientist Daily la Uingereza limebainisha.

Utafiti huo umebaini kwamba dawa za kupunguza maumivu kama Brufen zinaongeza uwezekano wa kusababisha kifo kwa zaidi ya asilimia 20, kutokana na shambulio la moyo ‘heart attack’.

Utafiti huo unashauri kuwa ni vyema wagonjwa ambao wanaandikiwa dawa za kutuliza maumivu, wakatumia kiwango kidogo cha dozi na kujitahidi kutozitumia mara kwa mara.

Pia, utafiti huo umeonya wanaopenda kununua dawa hizo wakati wowote kwenye maduka bila kufuata ushauri wa daktari.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Vidonge vya maumivu chanzo cha ongezeko la vifo vya ghafla. Vidonge vya maumivu chanzo cha ongezeko la vifo vya ghafla. Reviewed by Zero Degree on 10/02/2016 10:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.