Loading...

Brazil yapaa hadi nafasi ya pili katika viwango vipya vya FIFA, ..itazame orodha itakavyokuwa.

Argentina watabaki kileleni kwenye viwango vya FIFA siku ambayo msimamo mpya utakapotoka Nov. 24, lakini Brazil ndio imekuja vingine na inaonekana kuja kwa kasi na itapanda mpaka nafasi ya 2.

Brazil wangeweza kutwaa nafasi ya kwanza kama Argentina ingepoteza mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya Colombia siku ya Jumanne, lakini ushindi wa 3-0 uliwabakisha katika nafasi ya 1 mpaka sasa.

Brazil iliyokuwa chini ya kocha mpya Tite, hawajawahi kuongoza msimamo huo wa FIFA tangu muda mfupi kabla ya kombe la dunia la mwaka 2010. 

Waliwachapa Argentina mabao 3-0 wiki iliyopita kabla ya kuwafunga 2-0 mjini Peru. Hivyo nafasi hii ya sasa inamaanisha wanarejea katika nafasi ya juu kama hiyo tangu miaka 6 iliyopita.

MSIMAMO MPYA WA FIFA, Top 20 UTAKAVYOKUWA.
  1. Argentina
  2. Brazil
  3. Germany
  4. Belgium
  5. Chile
  6. Colombia
  7. France
  8. Portugal
  9. Uruguay
  10. Spain
  11. Switzerland
  12. Wales
  13. England
  14. Croatia
  15. Poland
  16. Italy
  17. Costa Rica
  18. Mexico
  19. Peru
  20. Ecuador
ZeroDegree.
Brazil yapaa hadi nafasi ya pili katika viwango vipya vya FIFA, ..itazame orodha itakavyokuwa. Brazil yapaa hadi nafasi ya pili katika viwango vipya vya FIFA, ..itazame orodha itakavyokuwa. Reviewed by Zero Degree on 11/17/2016 06:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.