Kiboko ya Manyika atua msimbazi.
KATIKA kuhakikisha inaimarisha nafasi ya makipa, uongozi wa klabu ya Simba upo katika mchakato wa kumrejesha kocha wa makipa, Mkenya Abdul Salim, kuwanoa makipa wa timu hiyo.
Wekundu wa Msimbazi hao hakuwa na kocha wa makipa, huku wakimtumia Adam Abdallah kwa ajili ya kuwanoa makipa wa timu hiyo, Vicent Angban, Peter Manyika na Denies Richard.
Salim alikuwepo msimu uliopita, ambapo alifanikisha kumuweka katika kiwango kizuri Manyika Jr na kupata nafasi mara kwa mara ya kucheza katika kikosi cha timu hiyo msimu uliopita, kabla ya kuondolewa.
Taarifa za uhakika kutoka kwa rafiki wa karibu wa kocha huyo nchini Kenya, zilizoifikia BINGWA zinasema kwamba, tayari vigogo wa Simba wanafanya mazungumzo kwa lengo la kumrejesha kuwanoa makipa wao.
Alisema baada ya kuondoka Simba, kocha huyo alipata nafasi ya kwenda nje na kurejea nchini Kenya kujiunga na AFC Leopards ya nchini humo kwa ajili ya kuwanoa makipa wa timu hiyo.
“Tayari Simba wapo katika mazungumzo na Salim na huenda mambo yakiwa mazuri atarudi Tanzania kuwafundisha makipa wa Simba,” alisema rafiki huyo.
BINGWA lilipomtafuta kocha huyo, alisema kwa sasa ana mkataba na timu ya AFC Leopards, hata hivyo, kama Simba wana nia ya kumhitaji yupo tayari kuja nchini kufundisha.
Simba imehakikisha inafanya maboresho katika nafasi ya benchi la ufundi kwa kuingia mkataba na kocha huyo pamoja na kuleta kipa mwingine atakayeleta ushindani na Angban ambaye kwa sasa mashabiki hawana imani naye.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Kiboko ya Manyika atua msimbazi.
Reviewed by Zero Degree
on
11/29/2016 11:35:00 AM
Rating: