Loading...

Mahakama yataka Neymar kufungwa jela kwa muda wa miaka miwili.

Waendesha mashtaka nchini Uhispania wamemtaka mshambuliaji wa Barcelona Neymar kuhudumia kifungo cha miaka miwili jela kufuatia kuhusika kwake katika kesi ya ufisadi kuhusu uhamisho wake kutoka klabu ya Santos nchini Brazil mwaka 2013.

Jaji Jose Perals pia ametaka aliyekuwa rais wa Barcelona sandro Rosell kuhudumia kifungo cha miaka mitano jela mbali na kupigwa faini ya Yuro milioni 7.2 kwa klabu hiyo.



Imetaka kutupiliwa mbali kwa mashtaka dhidi ya rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria bartomeu.

Rosell,Neymar na babake wanatarajwa kushtakiwa.


Kesi hiyo inatokana na malalamishi ya kundi la uwekezaji la Brazil DIS ,ambalo linamiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar na linadai lilipata fedha chache ikilinganishwa na zile lililotarajia.

Rosell alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mwaka 2014 kwa jukumu lake katika uhamisho huo na kutoa ushahidi mahakamani mnamo mwezi Februari pamoja na Bartomeu,Neymar na babake Neymar.

ZeroDegree.

Mahakama yataka Neymar kufungwa jela kwa muda wa miaka miwili. Mahakama yataka Neymar kufungwa jela kwa muda wa miaka miwili. Reviewed by Zero Degree on 11/23/2016 06:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.