Loading...

Man City wapata ushindi wa kusisimua dhidi ya Barcelona.

Manchester City wanahitaji kushinda mechi moja kufika hatua ya mtoano Ligi ya maingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wa kusisimua dhidi ya miamba ya Uhispania Barcelona.

Mechi hiyo ilichezewa uwanja wa Etihad.

Lionel Messi alifunga bao lake la 90 ligi hiyo ya mabingwa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Neymar na kuwaweka mbele Barca muda wa mapumziko ulipokuwa unakaribia.

Lakini mambo yalibadilika upesi kabla ya kipenga kupulizwa pale Sergi Roberto alipofanya kosa na Raheem Sterling akampa mpira Ilkay Gundogan ambaye alifunga kwa njia rahisi sana.

City, ambao walikuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Barcelona katika mechi sita, walianza kudhihirisha ubabe wao kuanzia wakati huo na frikiki ya Kevin de Bruyne ilimuumbua kipa Marc-Andre ter Stegen dakika ya 51.

Mpira wa Andre Gomes uligonga mwamba huku Barcelona wakisaka bao la kusawazisha lakini City walijihakikishia ushindi wa kusisimua dhidi ya klabu ya zamani ya meneja wao Pep Guardiola zikiwa zimesalia dakika 16 pale De Bruyne alipompa pasi Jesus Navas naye akatoa krosi iliyomfikia mshambuliaji Sergio Aguero, kabla ya kumfikia Gundogan aliyefunga.

City watafuzu kwa hatua ya 16 bora iwapo watashinda Borussia Monchengladbach ugenini Novemba 23.

Gladbach walitoka sare na Celtic.

Gundogan alifunga mabao mawili na kukamilisha 96% kati ya pasi 28 alizotoa.

MATOKEO Kamili: Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya:

KUNDI A
  • Basel 1-2 Paris Saint Germain
  • Ludo Razgd 2-3 Arsenal
KUNDI B
  • Besiktas 1-1 Napoli
  • Benfica 1-0 Dynamo Kiev

KUNDI C
  • Bor Monchengladbach 1-1 Celtic
  • Manchester City 3-1 Barcelona

KUNDI D
  • Atletico Madrid 2-1 FC Rostov
  • PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich
Manchester City walikuwa wameshinda mechi tano awali na Barcelona.

ZeroDegree.
Man City wapata ushindi wa kusisimua dhidi ya Barcelona. Man City wapata ushindi wa kusisimua dhidi ya Barcelona. Reviewed by Zero Degree on 11/02/2016 01:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.