Loading...

Michango ya maafa ya tetemeko la ardhi Kagera yafikia bilioni 5.4

Kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera imeishapokea zaidi ya shilingi Bilioni 5.4 hadi kufikia Novemba 10, mwaka huu ambayo ni michango ya wadau mbalimbali ambao ni pamoja na taasisi binafsi na zile za kiserikali, mashirika ya kimaifa, nchi marafiki inatotolewa kwa lengo la kukabili maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo na kusababisha madhara makubwa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea juhudi za kamati hiyo katika kukabiliana na madhara ya tetemeko,amesema kamati hiyo imeishatumia kiasi cha shilingi bilioni 1.1 kutokana na michango hiyo kwa ajili kukarabati miundombinu ambayo imeharibiwa na tetemeko ambayo ni pamoja na zahanati,vituo vya afya,shule za msingi na sekondari.

Aidha,mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuwapongeza waliochukua hatua ya kujenga upya nyumba zao ziliharibiwa na tetemeko,amesema kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera iko kwenye mchakato wa kuhakikisha makundi maalumu yenye uhitaji yanarejesha katika hali ya kawaida miundombinu ya nyumba zao za makazi iliyoharibiwa na tetemeko,amesema kamati hiyo tayari imeishafanya makubaliano na Kanisa la Pentekoste ambalo limeahidi kujenga nyumba za wenye uhitaji kwa awamu mbalimbali ambapo katika awamu ya kwanza kanisa hilo litajenga nyumba 370.

Nao baadhi ya wazee na wajane wameonyesha kutoridhishwa na utaratibu unaotumika wa kuyabainisha makundi yenye uhitaji,wakizungumza wamesema utaratibu wa kuyabaini makundi hayo kuwa unawabagua baadhi ya waathirika wa tetemeko wenye uhitaji.

ZeroDegree.
Michango ya maafa ya tetemeko la ardhi Kagera yafikia bilioni 5.4 Michango ya maafa ya tetemeko la ardhi Kagera yafikia bilioni 5.4 Reviewed by Zero Degree on 11/12/2016 12:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.