Loading...

Vyama vitatu vya siasa nchini vimefutiwa usajili.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi. 
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutowasilisha ripoti za ukaguzi wa hesabu za fedha.

Sababu nyingine ni kutokuwa na ofisi na kushindwa kuthibitisha kuwa na wanachama Zanzibar

Amevitaja vyama hivyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta) kilichokuwa kinaongozwa na James Mapalala na The Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) kilichokuwa kinaongozwa na Peter Mziray kama Rais Mtendaji.

Chama kingine kilichofutiwa usajili ni Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari kama Mwenyekiti taifa.



ZeroDegree.
Vyama vitatu vya siasa nchini vimefutiwa usajili. Vyama vitatu vya siasa nchini vimefutiwa usajili. Reviewed by Zero Degree on 11/09/2016 04:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.