Loading...

'Walimu marufuku kuvaa nguo fupi'

WALIMU wanawake wa shule za msingi na sekondari mkoani Tanga, wametakiwa kuacha kuvaa nguo fupi (vimini).

Mratibu wa Mandeleo ya Wanawake Kanda ya Kati (Inuka), David Msuya amesema nguo hizo zinakiuka maadili ya utumishi na kusababisha wanafunzi kushindwa kuzingatia masomo na kutumia muda mwingi kuwatazama wanapofundisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema tabia hiyo imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa kushusha ari ya wanafunzi kusoma.

Badala ya kuzingatia wanachofundishwa wanaishia kutazama namna ya uvaaji wa nguo za aina hiyo, alisema.

Alisema licha ya vimini, pia nguo nyingine ambazo zimekuwa zikiwapa wakati mgumu ni wale wanaovaa madela na baibui ambazo pia zimekuwa zikionyesha maungo kwa urahisi na kusababisha usumbufu kwa jamii.

“Uvaaji wa nguo fupi unasababisha wanafunzi kushindwa kuzingatia wanachokuwa wakifundishwa hasa wakati wanapokuwa wakiinama kwa sababu baadhi ya maungo yao ya mwili huonekana jambo ambalo linasababisha kuwaondolea umakini wa kusoma,” alisema.

Mratibu huyo alikemea suala la rushwa ya ngono hasa kwenye nafasi ndani ya halmashauri ikiwamo kitendo cha kupendelewa baadhi ya wakuu wa idara
ambao hawastahili.

Alisema hata usimamizi wa mitihani wa darasa la saba walimu wanaopangwa ni wale wale jambo ambalo huwavunja moyo watumishi wengine ambao hufanya kazi zao kwa weledi mkubwa.

ZeroDegree.
'Walimu marufuku kuvaa nguo fupi' 'Walimu marufuku kuvaa nguo fupi' Reviewed by Zero Degree on 11/18/2016 11:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.